Mgahawa wa Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya katika mji wa Najafu, unajiandaa kupokea mazuwaru wanaopita katika mkoa wa Najafu Kwenda Karbala kufanya ziara ya Arubaini.
Mgahawa unatoa huduma tofauti ikiwa ni pamoja na kugawa maelfu ya sahani za chakula kila siku, sambamba na huduma za afya kupitia kituo chake.
Mgahawa wa Ataba mbili tukufu unakituo cha Tablighi kwa wanaume na wanawake na sehemu ya ufundishaji wa kusoma Qur’ani tukufu.
Aidha kunasehemu maalum ya kupumzika na kulala mazuwaru na watumishi wa kujitolea, sehemu za kulala zipo za wanaume na wanawake, sehemu ya vyoo na sehemu ya kuswalia.
Mgahawa huu unaendeshwa kwa ushirikiano wa Atabatu Husseiniyya na Abbasiyya.