Kitengo cha mgahawa katika Atabatu Abbasiyya kimetangaza kuwa kimegawa zaidi ya sahani laki tatu za chakula ndani ya siku tisa.
Rais wa kitengo hicho bwana Aadil Hamami amesema “Mgahawa wa Atabatu Abbasiyya tukufu umegawa zaidi ya sahani laki tatu za chakula ndani ya siku tisa”.
Akabainisha kuwa: “Idadi hiyo imetolewa kuanzia mwezi mosi Safar hadi mwezi tisa na maji baridi ya kunywa pamoja na huduma zingine”.
Chakula kimetolewa kwa utaratibu maalum uliowekwa kupitia sehemu tatu zilizopangwa kwenye barabara zinazotumiwa na mazuwaru wengi.
Akasema: “Chakula hupikwa mapema kila siku na huwekwa kwenye vifungashio kwa ajili ya kugawa kwa mazuwaru watukufu, ambao wanakuja kwa wingi kufanya ibada ya ziara”.