Katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu anakagua maandalizi ya ziara ya Arubaini akiwa pamoja na mkuu wa mkoa wa Karbala

Maoni katika picha
Katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu Sayyid Mustafa Murtadha Dhiyaau-Dini akiwa na mkuu wa mkoa wa Karbala Sayyid Naswifu Alkhatwabi wamekagua maandalizi ya kupokea mazuwaru wa Arubaini ya Imamu Hussein (a.s).

Wametembelea vituo vya kutoa huduma vilivyo chini ya Ataba tukufu na mawakibu na kuangalia mahitaji yao.

Sambamba na kuangalia mikakati ya ulinzi na usalama iliyowekwa na watumishi wa Ataba kwa kushirikiana na vyombo vya usalama.

Hii ni sehemu ya ziara nyingi zinazofanywa na katika mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu kila siku wakati huu wa ziara ya Arubaini.

Mji mtukufu wa Karbala unashuhudia mamilioni ya watu wanaokuja kufanya ziara ya Arubaini ya Imamu Hussein, jambo linalowalazimu watumishi wa Ataba mbili tukufu kujiandaa kutoa hutuma mbalimbali ndani ya mji wa Karbala na kwenye barabara kuu zinazoingia Karbala kutokea (Najafu, Baabil, Husseiniyya na Bagdad).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: