Idara ya wahadhiri wa Husseiniyya tawi la wanawake inafanya harakati mbalimbali kwa mazuwaru wa Arubaini

Maoni katika picha
Idara ya wahadhiri wa Husseiniyya tawi la wanawake inafanya harakati mbalimbali zinazo husu wanawake wanaokuja kufanya ziara ya Arubaini katika mji mtukufu wa Karbala.

Kiongozi wa Idara hiyo bibi Taghrida Tamimi amesema “Idara inatoa mihadhara ya kidini na maelekezo mbalimbali, kupitia vituo tofauti vilivyojengwa kwa ajili ya kuhudumia mazuwaru, akasema: moja ya sehemu tunazotoa huduma ni kwenye jengo la Shekhe Kuleini upande wa Bagdad – Karbala”.

Akaongeza kuwa “Idara imeandaa ratiba maalum inayo husu watoto, sambamba na kuweka mashindano ya kielimu na kutoa zawadi kwa washindi”.

Kwa mujibu wa kiongozi wa idara chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu “Harakati hizi zinalenga kunufaika na ziara ya Arubaini”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: