Majmaa ya Qur’ani tukufu inaendesha program ya mchoraji wa Husseini kwa ajili ya maelekezo ya dini, kwenye barabara ya (Yaa Hussein).
Program hiyo inasimamiwa na Maahadi ya Qur’ani tukufu ya mji wa Najafu, chini ya Majmaa ya Qur’ani.
Kiongozi wa harakati za Qur’ani katika Maahadi Sayyid Zaidu Rimahi amesema “Program hii inahusu uchoraji na kupaka rangi picha zinazo elezea tukio la Karbala, kwa lengo la kufikisha ujumbe kwa mazuwaru hususan watoto kupitia njia hiyo, sambamba na kutengeneza bango zinazo elezea Maimamu wa Ahlulbait (a.s)”.
Akaongeza kuwa “Program hii inahusisha mihadhara ya Dini yenye mada tofauti, pamoja na kueleza utukufu wa ziara ya Arubaini”.