Kamati ya ufuatiliaji katika kitengo cha utumishi imeandaa shule kadhaa katika mji wa zamani kwa ajili ya kulala mazuwaru.
Mkuu wa idara huiyo bwana Haidari Abbasi Husseini amesema “Watumishi wetu wameandaa shule saba kwa ajili ya kulala mazuwaru wa Arubaini ya Imamu Hussein (a.s), shule hizo zimesafishwa na kufanyiwa ukarabati kama vile kupakwa rangi, kurekebisha umeme, vyoo na kuweka magodoro na shuka”.
Shule tatu zipo karibu na Atabatu Abbasiyya tukufu, watu (4500) wanaweza kulala katika shule hizo.
Akasema “Kuna hoteli imeandaliwa rasmi kwa ajili ya kulala watumishi wa kujitolea wapatao (2000)”.
Kitengo cha utumishi kupitia idara zake kinafanya kazi kubwa ya kuhudumia mazuwaru wa Arubaini katika mji wa Karbala saa (24) kila siku bila kupumzika.