Majmaa ya Qur’ani tukufu imefungua majlisi za maukibu ya kiongozi wa wasomaji, iliyohudhuriwa na idadi kubwa ya mazuwaru.
Majlisi ya ufunguzi imehudhuriwa na rais wa Majmaa ya Qur’ani Dokta Mushtaqu Ali na mkuu wa kituo cha miradi ya Qur’ani Sayyid Hasanaini Halo na watumishi wa kituo walimu, wanafunzi na viongozi wa chuo kikuu cha Al-Ameed.
Muimbaji wa kaswida za Husseiniyya bwana Ammaar Kinani ameipamba majlisi hiyo kwa kuimba kaswida za kuomboleza zilizo amsha hisia ya machonzi, huku Qur’ani ya ufunguzi ikisomwa na Muhammad Ridha Zubaidi.
Jioni ya Jumamosi Maukibu itaanza kufanya shughuli mbalimbali.