Hema la bibi Ruqayya (a.s) linalo simamiwa na Maahadi ya Qur’ani tukufu tawi la wanawake, limepata muitikio mkubwa kutoka kwa mazuwaru wenye umri mdogo.
Kiongozi wa Maahadi hiyo bibi Manaar Jaburi amesema “Hema limevutia mazuwaru wenye umri mdogo, wameandaliwa ratiba ya Qur’ani kwa lengo la kuonyesha umuhimu wao katika kuhuisha maadhimisho ya Imamu Hussein (a.s)”.
Akaongeza kuwa “Ratiba inamambo ya kielimu kwa njia nyepesi, kwa kuunda makundi ya kubadilishana elimu kwa lengo la kujenga moyo wa kushirikiana baina yao, sambamba na michezo mbalimbali na ugawaji wa zawadi kwa wanaofanya vizuri”.
Hema la bibi Ruqayya (a.s) limewekwa katika Maukibu ya Ataba mbili tukufu kwenye barabara ya (Yaa Hussein / nguzo namba 208), Maahadi imeandaa ratiba mbalimbali za Qur’ani tukufu kwenye vituo tofauti, vilivyo wekwa kwenye barabara zinayotumiwa na mazuwaru wengi wa Abu Abdillahi Hussein (a.s)”.