Majmaa ya Qur’ani imekamilisha maandalizi ya kituo maalum cha Qur’ani tukufu, chenye jukumu la kuwatambulisha msahafu uliochapishwa na Aatabatu Abbasiyya kwa mazuwaru wa Arubaini.
Kituo hicho kinasimamiwa na mkuu wa kitengo cha uchapishaji wa Qur’ani tukufu chini ya Majmaa Shekhe Dhiyaau-Dini Zubaidi, amesema: “Kituo kitatoa nafasi kwa mazuwaru watukufu wa Arubaini ya kushiriki kwenye uandishi wa msahafu mtukufu”.
Akaongeza kuwa “Kituo kipo kwenye barabara inayotumiwa na mazuwaru wengi ya Najafu – Karbala, katika chuo kikuu cha Al-Ameed, mkabala na nguzo namba (1237), kinapokea mazuwaru watukufu saa ishirini na nne kila siku hadi kipindi cha ziara ya Arupaini kitakapoisha”.