Idara ya Masayyid.. inatoa huduma tofauti kwa mazuwaru wa Arubaini

Idara ya Masayyid inashiriki katika kuhudumia mazuwaru wa Arubaini ya Imamu Hussein (a.s).

Wahudumu wa idara hiyo wanafanya kazi mbalimbali, kwa mujibu wa maelezo ya mmoja wa wajumbe wake Sayyid Ali Mamitha.

Akasema: “Kazi tunazo fanya wakati wa ziara ni pamoja na kusafisha ndani ya uwanja wa haram mara tatu kila siku na kuweka misahafu na vitavu vya dua kwenye kabati za vitabu”.

Akaendelea kusema: “Wahudumu wa idara yetu wanashiriki kutoa huduma kwenye mawakibu zilizo chini ya Ataba tukufu sambamba na kufungua maukibu maalum ya idara karibu na haram tukufu”.

Akafafanua kuwa “Masayyid wanashiriki pia kuratibu matembezi ya mawakibu zinazo ingia Ataba tukufu, sambamba na mazuwaru”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: