Kitengo cha mahusiano kinaendelea na huduma ya uokozi katika ziara ya Arubaini

Kitengo cha uhusiano kinatoa huduma ya uokozi kwa mazuwaru wa Arubaini ya Imamu Hussein (a.s), kiongozi wa idara ya shule na msimamizi mkuu wa vituo vya afya Sayyid Muhammad Yasiri amesema “Watumishi wa idara ya mahusiano ya vyuo na shule na wafanyakazi wa kujitolea, wanatoa huduma kwa mazuwaru muda wote, wanafanya kazi kwa zamu tatu”.

Akaongeza kuwa “Kila zamu ya kazi inasaa nane, wanajumla ya gari tisa za wagonjwa, zitaongezeka kidogokidogo kutokana na kuongezeka kwa idadi ya mazuwaru, zitafika hadi gari kumi na nne siku chache zijazo”.

Akasisitiza kuwa “Kazi inaendelea kama ilivyo pangwa”, akasema kuwa “Wahudumu wetu wamevaa sare maalum kwa ajili ya kuwafanya watambulike kwa urahisi”
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: