Pamoja na wingi wa mazuwaru.. kitengo kinachosimamia uwanja wa katikati ya haram mbili kinaendelea na kazi yake

Watumishi wa kitengo kinacho simamia uwanja wa katikati ya haram mbili kinaendelea na kazi zake za usafi, kugawa maji ya kunywa, kubeba mazuwaru na kuratibu matembezi ya mazuwaru wa Arubaini.

Rais wa kitengo hicho Sayyid Naafii Mussawi amesema: “Pamoja na msongamano mkubwa wa mazuwaru, watumishi wetu wanaendelea na kazi ya kusafisha eneo hilo wakati wote na kugawa maji baridi ya kunywa kwa mazuwaru kupitia vituo vya kugawa maji vilivyopo karibu na Atabatu Abbasiyya tukufu”.

Akafafanua kuwa “Tunatoa huduma katika uwanja wa katikati ya haram mbili na kwenye maeneo yaliyopauliwa na katika barabara zinazo zunguka eneo hilo au zinazo elekea Ataba mbili tukufu, bila kusahau chochoro za mji wa zamani”.

Akaongeza kuwa “Kazi hizo ni sehemu ya mkakati wa huduma za ziara ya Arubaini, ambampo kuna huduma mbalimbali za kibinaadamu zinazo tolewa”.

Kwa mujibu wa maelezo ya Mussawi “Kitengo hicho kimeandaa jopo maalum la mafundi kwa ajili ya kutengeneza gari yeyote itakayo haribika wakati wa kazi, sawa iwe ya maji au taka”. Akasisitiza kuwa “Tuna hakikisha eneo hili linakua safi wakati wote”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: