Mjumbe wa kamati kuu ya Atabatu Abbasiyya tukufu Mheshimiwa Sayyid Liith Musawi amesisitiza umuhimu wa maonyesho ya Qur’ani yanayofanywa na Majmaa ya Qur’ani katika Ataba tukufu.
Amesema “Maonyesho ya Qur’ani yanasaidia kulainisha nyoyo za mazuwaru wa bwana wa mashahidi (a.s) na kuhudhurisha utamaduni wa kushikamana na vizito viwili katika njia hii tukufu ya Husseiniyya”.
Akaongeza kuwa “Tunathamini kazi zinazo fanywa na Maahadi ya Qur’ani tukufu kwa kuweka maonyesho haya kwenye njia za (Yaa Hussein)”.
Maonyesho yanasimamiwa na Maahadi ya Qur’ani tukufu katika mji wa Najafu, chini ya Majmaa ya Qur’ani katika Atabatu Abbasiyya tukufu”.