Mheshimiwa Sayyid Swafi amesisitiza umuhimu wa kuhudumia mazuwaru wa Arubaini

Mheshimiwa kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya tukufu Sayyid Ahmadi Swafi, amesisitiza umuhimu wa kutoa huduma bora kwa mazuwaru wa Arubaini wanaokuja Karbala kutoka kila sehemu ya dunia.

Amesema hayo alipotembelea maukibu ya Ummul-Banina (a.s) iliyochini ya chuo kikuu cha Al-Ameed na maukibu zingine za Ataba tukufu, na kuangalia huduma wanazopewa mazuwaru.

Katika ziara hiyo Mheshimiwa amekutana na rais wa chuo Dokta Muayyad Ghazali na wasimamizi wa maukibu ya Ummul-Banina (a.s), amepongeza kazi nzuri wanayo fanya na akatoa wito wa kuendelea kuhudumia mazuwaru wa Abu Abdillahi Hussein (a.s).

relatedinner
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: