Atabatu Abbasiyya tukufu imetoa chapisho jipya la kuongoza mazuwaru wa Arubaini, chapisho hilo linaramani ya barabara zote za mji wa zamani.
Kiongozi wa idara ya kitengo kinacho simamia uwanja wa katikati ya haram mbili Sayyid Muntadhar Muhammad Hamza amesema: “Kutokana na ufuatiliaji wetu endelevu na kuangalia mafanikio na madhaifu katika utekelezaji wa ziara, tumeamua kuandika chapisho jipya lenye ramani ya barabara zote za mji wa zamani”.
Akaongeza kuwa “Tumeandaa watu maalum kwa ajili ya kuongoza mazuwaru na kuwarahisishia kufika kwenye maeneo wanayokusudia”, akabainisha kuwa “Chapisho hili litafanyiwa maboresho kila wakati kwa kuongezwa kwenye ramani jengo lolote litakalo jengwa katika mji huu”.
relatedinner