Mawakibu za Husseiniyya zinahuisha kumbukumbu ya Arubaini

Asubuhi ya Jumatatu mwezi 16 Safar mawakibu za Husseiniyya zinazokuja Karbala kutoka miji tofauti ya Iraq na duniani kwa ujumbla zimehuisha kumbukumbu ya Arubaini.

Mawakibu zinamiminika katika malalo ya bwana wa mashahidi (a.s), huku zikiimba kaswida za kuomboleza zinazo amsha hisia za huzuni, kisha zinaelekea katika malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) kukamilisha shughuli za uombolezaji.

Mawakibu za waombolezaji zinatoka kwenye mikoa tofauti ya Iraq na nje ya Iraq, zitaendelea kuwasiri hadi mwezi ishirini Safar, siku ambayo ndio kilele cha ziara ya Arubaini, kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa na kitengo cha maadhimisho na mawakibu Husseiniyya, Mawakibu zinaingia kwa kufuata utaratibu uliowekwa kuanzia siku ya kwanza hadi ya mwisho, kwa namna ambayo hazitatizi shughuli za mazuwaru watukufu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: