Tambua sehemu za vituo vya huduma za afya vilivyo chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu

Atabatu Abbasiyya tukufu imetaja sehemu vilipo vituo vyake vya afya vipatavyo (16), vinavyotoa matibabu kwa mazuwaru wa Arubaini katika sehemu mbalimbali za mji wa Karbala.

Vinatoa huduma ya matibabu kupitia madaktari bingwa.

Relatedinner

Zifuatazo ni sehemu ambazo vinapatikana vituo vya afya:

 • 1- Kituo cha Ummul-Banina (a.s) mkabala na mlango wa Imamu Muhammad Aljawaad (a.s) kaskazini ya Ataba tukufu.
 • 2- Kituo cha Swidiqatu-Twahirah (a.s) cha wanawake – mkabala na mlango wa Imamu Muhammad Aljawaad (a.s) upande wa kusini ya Ataba tukufu.
 • 3- Hospitali ya Shahidi Muhammad Radhi (r.a) mlango wa Bagdad katika mlango wa Hashimiyya.
 • 4- Kituo cha bibi Narjisi (a.s) – Mlango wa Kibla ya Abbasi (a.s).
 • 5- Kituo cha Imamu Mussa Alkadhim (a.s) – Mlango wa Kibla ya Abbasi (a.s).
 • 6- Kituo cha Imamu Ali Alhaadi (a.s) – mkabala na mlango wa Alqami katika uwanja wa Qassim upande wa mashariki ya Atabatu Abbasiyya tukufu.
 • 7- Kituo cha bibi Ruqayya (a.s) cha wanawake – mkabala na mlango wa Alqami katika uwanja wa Qassim upande wa mashariki ya Ataba tukufu.
 • 8- Kituo cha Imamu wa zama (a.f) – Maqaam ya Imamu Mahadi (a.f).
 • 9- Kituo cha bibi Zainabu (a.s) – cha wanawake- kitengo cha mgahawa wa Ataba tukufu.
 • 10- Mgahawa wa nje – katika mgahawa wa nje barabara ya Najafu – Karbala.
 • 11- Kituo cha jengo la Shekhe Kuleini – katika jengo la Shekhe Kuleini (q.s) barabara ya Bagdad – Karbala.
 • 12- Kituo cha Majmaa Ilmi – kwenye jingo la Alqami barabara ya Hilla – Karbala.
 • 13- Kituo cha chuo kikuu cha Al-Ameed – katika chuo kikuu cha Al-Ameed barabara ya Najafu – Karbala.
 • 14- Kituo cha Imamu Hassan Askariy (a.s) – karibu na uzio wa Imamu Mussa Alkaadhim (a.s)-.
 • 15- Kituo cha Imamu Sajjaad (a.s) katika ukumbi wa haram tukufu.
 • 16- Vituo viwili kwenye uwanja wa katikati ya haram mbili tukufu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: