Uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu baada ya Adhuhuri ya Jumatatu umefanya majlisi ya kumbukumbu ya Arubaini ya Imamu Hussein (a.s) na kuhudhuriwa na kiongozi mkuu wakisheria Mheshimiwa Sayyid Ahmad Swafi (d.i) na watumishi wa malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s).
Majlisi hizo zitadumu kwa muda wa siku tano, imefunguliwa kwa Qur’ani tukufu iliyofuatiwa na mawaidha kutoka kwa Shekhe Abdullahi Dujaili, ameeleza Maisha ya Imamu Hussein (a.s), na mambo muhimu yaliyotokea katika historia yake tukufu.
Ikahitimishwa kwa tenzi za kuomboleza zilizo elezea kifo cha bwana wa vijana wa peponi na yaliyomtokea yeye, watu wa nyumbani kwake na wafuasi wake (a.s),
Atabatu Abbasiyya tukufu kwenye kila tukio linalo husu kumbukumbu ya kifo cha Ahlulbait (a.s), huandaa ratiba ya kuomboleza tukio hilo.