Katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu Sayyid Mustwafa Murtadha Dhiyaau-Dini amefanya ziara ndani ya mji wa zamani kukagua maandalizi ya ziara ya Arubaini.
Mheshimiwa katibu mkuu ametembelea vituo vyote vya Atabatu Abbasiyya pamoja na baadhi ya mawakibu na kusikiliza mahitaji yao.
Mji wa Karbala kwa sasa unapokea mamilioni ya watu kutoka mikoa tofauti ya Iraq na duniani kwa ujumla wanaokuja kufanya ziara ya Arubaini.
Atabatu Abbasiyya imeandaa ratiba maalum ya utoaji wa huduma mbalimbali kwa kushirikiana na idara za serikali.