Wanaonyesha kuridhishwa na malikale wanazo shuhudia.. mazuwaru wa Arubaini wanamiminika kwenye makumbusho ya Alkafeel

Maelfu ya mazuwaru wanaingia kwenye makumbusho ya Alkafeel iliyopo ndani ya haram ya Abbasi (a.s) kuangalia malikale.

Rais wa kitengo cha makumbusho Swadiqu Laazim amesema: “Makumbusho inapokea maelfu ya watu kutoka mikoa yote ya Iraq na duniani kwa ujumla” akasema: “Mazuwaru wanaonyesha kufurahishwa na malikale za thamani tulizonazo na jinsi zilivyo pangwa”.

Mazuwaru wanavutiwa zaidi na malikale zinazohusu haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s), kama milango ya zamani, mabaki ya haram yaliyotunzwa baada ya kushambuliwa na utawala wa kidikteta uliopinduliwa, akasema kuwa makumbusho ipo wazi saa (24) katika siku hizi za ziara ya Arubaini.

Makumbusho ya Alkafeel ndio makumbusho ya kwanza katika makumbusho za Ataba za Iraq, ilifunguliwa mwaka (2009m) katika kumbukumbu ya kuzaliwa bibi Zainabu (a.s), inamalikale nyingi, baadhi historia yake inarudi mamina ya miaka.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: