Kitengo cha habari kimefungua mlango wa kujiandikisha kufanyiwa ziara ya Arubaini

Kitengo cha Habari katika Atabatu Abbasiyya kimefungua mlango wa kujiandikisha kufanya ziara ya Arubaini kwa niaba ya waumini walio ndani na nje ya Iraq.

Kiongozi wa idara ya teknolojia na taaluma ya mitandao Sayyid Haidari Twalibu Abdul-Amiir amesema: “Usajili wa kufanyiwa ziara kwa niaba unafanyika kupitia ukurasa wa ziara kwa niaba (https://alkafeel.net/zyara) uliopo kwenye mtandao wa kimataifa Alkafeel (https://alkafeel.net/Apps/Arabic) ambao ni mtandao rasmi wa Atabatu Abbasiyya tukufu, Pamoja na App zake zinazopatikana kwenye simu-ganja za kisasa (smartphone)”.

Akaongeza kuwa “Ziara hizo zitafanywa na wahudumu wa malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s), wakiwemo masayyid na watu wengine, watafanya ziara kwa niaba ya wapenzi na wafuasi wa Ahlulbait (a.s) wa dunia nzima.”

Mlango wa kujisajili kwa ajili ya ziara hiyo umefunguliwa toka siku kumi zilizo pita, amesema kuwa “Tumefanya hivyo kwa ajili ya kutoa nafasi kubwa zaidi ya kujisajili kupitia mitandao yote”, akafafanua kuwa “Ibada ya ziara itafanywa ndani ya haram ya Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s), watafanyiwa ziara maalum ya Arubaini, swala ya ziara na dua, watu wote watakao jisajili”.

Mtandao wa Kimataifa Alkafeel (https://alkafeel.net/Apps/Arabic/).

App ya Alkafeel (Atabatu Abbasiyya tukufu) – Android& IPhone.

Kupakua App ya Alkafeel bure – IPhone &Android
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: