Kwa urefu wa makumi ya kilometa.. barabara ya (Yaa Hussein) imeshuhudia swala ya jamaa ndefu zaidi iliyo ongozwa na makumi ya maimamu katika wanafunzi wa hauza

Barabara ya (Yaa Hussein) jioni ya Jumatano upande wa (Najafu – Karbala), imeshuhudia swala ya jamaa iliyo ongozwa na makumi ya maimamu katika wanafunzi wa hauza, jambo hili limekua likifanywa kwa miaka kumi mfululizo.

Mjumbe wa kamati ya kuandaa swala hiyo Sayyid Muhammad Hablu-Matiin amesema “Swala inamakumi ya kilometa zilizo gawanywa kwenye vituo tofauti, lengo la swala hii ni kujibu tuhuma wanazopewa wafuasi wa madhehebu ya Ahlulbait (a.s) na mazuwaru, ya kwamba hawajali swala, hutembea wakati wa swala bila kuswali”. Akaongeza kuwa “Swala ya jamaa ndefu inamatokea chanya mengi, yanayo ungwa mkoni na riwaya nyingi, miongoni mwa faida zake ni namna mazuwaru na mawakibu Husseiniyya wanavyo ukimbilia”.

Akasema kuwa “Barabara ya (Yaa Hussein) inamakundi matatu, kundi la kwanza ni watu wanaotaka thawabu kwa kutembea kwenda kwa bwana wa vijana (a.s), kundi la pili ni mawakibu za kutoa huduma ya chakula kwa mazuwaru, na kundi la tatu ni wanafunzi wa hauza wanaotoa chakula cha roho kwa mazuwaru, ikiwa ni pamoja na kuwahimiza kuswali swala ya jamaa ya pamoja”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: