Kitengo cha maarifa kinashiriki katika vituo vya kijana wa Alkafeel

Kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu kimeshiriki kwenye maonyesho ya vitabu yanayofanywa kwa mara ya tatu kwenye kituo cha (vijana wa Alkafeel kutoka vyuo vikuu na shule za Iraq” katika barabara ya, Yaa Hussein.

Kiongozi wa idara ya Habari katika kitengo hicho bwana Ali Baasim amesema “Tawi la kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu limeshiriki likiwa na vitabu vingi kutoka kwenye vituo vyake”.

Akaongeza kuwa “Ushiriki huu unasaidia kufikisha vitabu kwa idadi kubwa ya mazuwaru wa Arubaini, na kuchangia katika harakati za kielimu na kitamaduni”.

Kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu kinatoa huduma za kielimu kwa mazuwaru wa Arubaini kwenye mikoa ya (Karbala, Basra, Dhiqaar na Hilla) kupitia vituo vya turathi vilivyo chini yake kwenye mikoa hiyo.

Rais wa kitengo cha maarifa Shekhe Ammaari Hilali amesema “Kitengo chetu hutumia ziara ya Arubaini kutoa elimu kwa jamii, kusambaza turathi za kiislamu na kutoa huduma mbalimbali kwa mazuwaru watukufu”.

Akaongeza kuwa “Kuna maukibu ya kutoa huduma katika mkoa wa Dhiqaar inayo simamiwa na idara ya kituo cha turathi za kusini, na maukibu nyingine sawa na hiyo katika mkoa wa Baabil, inasimamiwa na kituo cha turathi za Hilla, kituo cha turathi za Basra kinagawa aina tofauti za chakula katika maeneo ya mpakani, na kinaharakati mbalimbali za kitamaduni kama vile (kongamano la kutoka baharini hadi mtoni)”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: