Kwa ushiriki wa zaidi ya watoa huduma wa kujitolea 1100.. idara ya madaktari inafanya kazi kubwa ya kuhudumia mazuwaru wa Arubaini

Idara ya madaktari chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu siku ya Alkhamisi, imeongeza huduma zake kwa kuwa na madaktari zaidi ya (1100) wanaojitolea kuhudumia mazuwaru wa Arubaini.

Mkuu wa idara ya madaktari Sayyid Aadil Saadi Jihadi amesema “Tumejenga vituo (19) vya afya katika njia za kuingia hapa mkoani, maeneo yanayo zunguka haram tukufu na ndani ya haram, sambamba na kufungua hospitali maalum kwa ajili ya kutoa huduma za haraka kabla ya kumpeleka mgonjwa kwenye hospitali kubwa ambako anaweza akachelewa kufika kwa sababu ya msongamano wa mazuwaru”.

Atabatu Abbasiyya tukufu imeandaa ratiba maalum ya afya kupitia vitengo na idara, mawakibu za kutoa huduma, na hospitali ya rufaa Alkafeel.

Akaongeza kuwa “Kuna ushirikiano mzuri na idara ya afya ya mkoa pamoja na idara ya dharura katika wizara ya afya ambayo imetupatia vifaa-tiba na gari za wagonjwa”.

Akafafanua kuwa “Katika utekelezaji wa jukumu hili wanashiriki madaktari (650) wa jinsia zote mbili, huku madaktari (450) wakitoa huduma za uokozi na huduma ya kwanza kwenye maeneo mbalimbali na ndani ya haram tukufu”.

Akaendelea kusema “Kuna kikosi cha uokozi katika eneo la mji wa zamani, kinajukumu la kusaidia wagonjwa wanaohitaji huduma ya upasuaji kisha wanapelekwa kwenye hospitali ya karibu”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: