Mawakibu za matam zinahuisha utiifu wao kwa Hussein (a.s)

Asubuhi ya Alkhamisi, mwezi kumi na nane Safar (1444h), zimeanza kumiminika katika mji wa Karbala mawakibu za kuomboleza (za matam) zikiwa zimejaa huzuni na majonzi.

Uingiaji wa mawakibu hizo unafuata ratiba iliyoandaliwa na kitengo cha maadhimisho na mawakibu Husseiniyya chini ya Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya.

Matembezi ya mawakibu hizo yanaanzia kwenye jukwaa lililopo katika barabara ya Kibla ya Imamu Hussein (a.s) hadi ndani ya malalo yake tukufu kisha wanatoka na kuelekea kwenye malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) wakipitia katika uwanja wa katikati ya haram mbili tukufu.

Imeanzishwa njia maalum ya kupita mawakibu bila kuleta usumbufu kwa mazuwaru, sambamba na kuzingatia nyakati za swala, kila panapo adhiniwa harakati zote za mawakibu zinasimama na watu wote wanaenda kuswali kwa mujibu wa maelezo ya rais wa kitengo cha maadhimisho Sayyid Aqiil Yaasiri.

Akaongeza kuwa “Kitengo cha maadhimisho na mawakibu Husseiniyya kilianza mapema kufanya maandalizi ya ziara ya Arubaini ya Imamu Hussein (a.s), kwa ajili ya kuhakikisha ziara inafanyika kwa amani na utulivu”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: