Harakati mbalimbali zinafanywa na shule ya Fatuma binti Asadi katika njia ya mazuwaru

Shule ya Fatuma binti Asadi (a.s) chini ya idara ya shule za Dini Alkafeel za wasichana, inafanya harakati mbalimbali kwa wanawake na watoto.

Kiongozi wa idara hiyo bibi Bushra Kinani amesema “Tunaprogram ya (Mishumaa katika njia ya Ruqayya) Qur’ani inayoelekezwa kwa watoto, ikiwa ni pamoja na kuwafundisha usomaji sahihi wa Surat Fat-ha, usimuliaji wa visa, usomaji wa aya za Qur’ani na mashairi yanayohusu kuwapenda Ahlulbait (a.s), kisha kufanya majlisi ya kuomboleza ya watoto”.

Akaongeza kuwa “Watoto wote wanaoshiriki kwenye ratiba hupewa zawadi baada ya kukamilisha ratiba”.

Ameongea kuhusu ratiba ya (Katika mwenendo wa Qur’ani) inayo husu wanawake kuwa “Imejikita katika kufundisha usomaji sahihi wa surat Fat-ha kwa mazuwaru watukufu, na kugawa kadi za ubora kwa waliosoma vizuri surat Fat-ha”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: