Kitengo cha maadhimisho na mawakibu Husseiniyya chini ya Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya kimetangaza kuwa jumla ya maukibu (12500) zimeshiriki katika kuhuisha ziara ya Arubaini hapa Karbala.
Kitengo kikafafanua kuwa “Maukibu za kigeni zilizo shiriki zipo (300) kutoka nchi cha kiarabu na kiajemi”.
Wakaendelea kusema “Mwaka huu tumekua na maukibu ya kutoa huduma kutoka nchi ya Palestina, pamoja na mawakibu zingine kutoka nchi za (China, Ujerumani, Holandi, Swiden, Naijeria, Iran, India na Pakistani)”.
Taarifa inasema kuwa “Kuna ubinaadamu wa hali ya juu na ushirikiano mkubwa baina ya mawakibu, vyombo vya ulinzi na usalama na udara za uratibu, sambamba na kuwekwa utaratibu ambao umezuwia msongamano baina yao”.