Inaposikika sauti ya adhana, sauti ya kuwaita watu kwa Allah, mazuwaru husimama na kuswali, wakienzi msimamo wa bwana wa mashahidi (a.s) na wafuasi wake walipo simama kuswali wakati wanarushiwa mishale.
Mmoja wa wahudumu wa maukibu anasema: “Kutokana na kauli ya Mwenyezi Mungu mtukufu ndani ya kitabu chake isemayo (Hakika swala kwa waumini imekua na wakati maalum) na usia wa Imamu Swadiq (a.s) usemao (Uombezi wetu hataupata mvimu wa kuswali).
Waombolezaji wa Ahlulbait (a.s), mazuwaru na watoa huduma kwenye mawakibu wanazingatia sana kuswali kwa wakati”, akaongeza kuwa “Wanafanya hivyo kama kuonyesha kwa vitendo yale aliyotaka Imamu Hussein (a.s) kufundisha kwa wafuasi na wapenzi wake”.
Ataba mbili tukufu kupitia kitengo cha maadhimisho na mawakibu Husseiniyya, zimeandaa sehemu kubwa kwa ajili ya swala na wamepangwa mashekhe maalum kwa ajili ya kuswalisha.