Hongera watu wa Qur’ani.. program mpya inayofanywa na Maahadi ya Qur’ani tawi la wanawake

Maahadi ya Qur’ani tukufu tawi la wanawake inafanya program mpya kwa jina la (Hongera watu wa Qur’ani), program maalum kwa mazuwaru wa kike.

Kiongozi wa Maahadi bibi Manaar Jaburi amesema “Hii ni program maalum kwa mazuwaru wa Imamu Hussein (a.s) waliohifadhi kitabu cha Mwenyezi Mungu mtukufu, kamati ya wasomi wa Qur’ani inauliza maswali kulingana na kiwango alicho hifadhi msichana anaeulizwa, kisha anapewa zawadi maalum kwa kuhifadhi kwake Qur’ani tukufu”.

Maahadi ya Qur’ani chini ya Atabatu Abbasiyya inafanya kila iwezalo katika kuhudumia mazuwaru, inahema (7) za usomaji wa Qur’ani katika barabara zinazo elekea Karbala.

Akaongeza kuwa “Program hii inalenga kutoa zawadi kwa wasichana waliohifadhi Qur’ani, na kuonyesha umuhimu wao katika jamii, sambamba na kuhimiza wasichana umuhimu wa jambo hilo tukufu”.

Akaendelea kusema “Maahadi imeandaa program tofauti zinazo husu mazuwaru watukufu, ikiwemo program hii”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: