Muwakilishi wa wakristo wa Othodox nchini Hispania na Ureno amesema: Huduma zinazotolewa hapa hazifikiriki

Muwakilishi wa wakristo wa kanisa la Othodox nchini Hispania na Ureno Rokhiliyu Sathkabo amesema kuwa huduma na ukarimu unaoshuhudiwa hapa Karbala ni wa kiwango cha juu kabisa kiasi ambacho haufikiriki.

Ameyasema hayo alipo tembelea Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya siku ya Ijumaa, akaongeza kuwa “Mara ya kwanza nilikuja Karbala kushiriki kwenye kongamano la Imamu Hussein (a.s) miaka minne iliyopita, baada ya kupewa mualiko na taasisi ya Ahlulbait (a.s) nchini Hispania, kuanzia mwaka huo nimekua na ham ya kuja Karbala kushiriki kwenye tukio hili la ziara ya Arubaini”.

Akaongeza kuwa “Kuna ushirikiano mkubwa sana baina ya watu, jambo ambalo halipo kwenye maeneo mengine, lakini ziara ya Imamu Hussein inaumaalum wa pekee ndani ya moyo”.

Akaendelea kusema “Katika nchi yetu kuna ukarimu lakini sio kwa kiwango hiki, hakika ukaribu wa Karbala haufikiriki”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: