Atabatu Abbasiyya yahitimisha majlisi za kuomboleza zilizofanywa wakati wa ziara ya Arubaini ya Imamu Hussein (a.s)

Uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu leo siku ya Ijumaa, umehitimisha majlisi za kuomboleza zilizokua zinafanywa ndani ya ukumbi wa utawala katika kumbukumbu ya Arubaini ya Imamu Hussein (a.s), na kuhudhuriwa na kiongozi mkuu wa kisheria Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi (d.i) na baadhi ya watumishi wa malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s).

Majlisi hiyo imedumu kwa muda wa siku nne, chini ya uhadhiri wa Shekhe Abdullahi Dujaili, amekua akiongea kuhusu uhai wa Imamu Hussein (a.s), na mambo muhimu yaliyotokea katika historia yake tukufu.

Majlisi ilikua inapambwa na tenzi za kuomboleza zilizo amsha hisia za huzuni na majonzi, kutokana na kifo cha bwana wa vijana wa peponi na yaliyo watokea watu wa nyumbani kwake (a.s) na wafuasi wake.

Atabatu Abbasiyya tukufu kwenye kila tukio linalo husu kumbukumbu ya kifo cha Ahlulbait (a.s) huandaa ratiba maalum ya uombolezaji.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: