Kwa namba.. katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu ameeleza huduma zilizotolewa katika ziara ya Arubaini

Katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu Sayyid Mutwafa Murtadha Dhiyaau-Dini ameeleza huduma zilizo tolewa na Atabatu Abbasiyya wakati wa ziara ya Arubaini hadi siku ya 19 Safar mwaka 1444h.

Mheshimiwa katibu mkuu katika ujumbe wake kwa vyombo vya Habari, ametaja huduma zilizotolewa na Atabatu Abbasiyya wakati wa ziara ya Arubaini pamoja na idadi ya mawakibu zilizo shiriki, ambapo zimefika 14500, zikiwemo maukibu 300 kutoka nchi za nje.

Idadi ya sahani za chakula zilizo tolewa kwa mazuwaru wa Arubaini ndani ya mji wa Karbala zimefika 4,481,377. Kwa mujibu wa maelezo ya katibu mkuu.

Akasema: “Tulisajili watoa huduma wa kujitolea 16384 wakati huu wa ziara ya Arubaini”, akaongeza kuwa “Jumla ya gari 805 za aina na ukubwa tofauti zimeshiriki kubeba mazuwaru na kutoa huduma”.

Akaendelea kusema “Tumegawa maji grasi 19,849,500 na vipande vya barafu 41000, maji tuliyozalisha na kuyasambaza karibu lita milioni nne”.

Kuhusu huduma za afya amesema: “Gari za wagonjwa 22 zimeshiriki kutoka huduma za afya, tulikua na vituo vya afya 54 vya kutembea na vya kujengwa katika mji wa Karbala”.

Vituo vya huduma za kitamaduni na kidini vipo 129 katika mji wa Karbala na kwenye barabara zinazokuja Karbala.

Akasema “Tumeweka vituo 35 vya kuelekeza watu waliopotea katika mji wa Karbala na kwenye njia zinazo elekea Karbala”.

Akasema kuwa jumla ya taasisi za Habari 190 zimeshiriki na magazeti 500 yameandika kuhusu ziara ya Arubaini, taasisi za Habari 300 zimepewa makazi na Ataba tukufu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: