Atabatu Abbasiyya yahitimisha majlisi za kuomboleza kumbukumbu ya Arubaini ya Imamu Hussein (a.s)

Uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu leo siku ya Jumamosi umehitimisha majlisi za kuomboleza zilizokua zinafanywa ndani ya ukumbi wa utawala katika kumbukumbu ya Arubaini ya Imamu Hussein (a.s), na kuhudhuriwa na kiongozi mkuu wa kisheria Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi na baadhi ya wahudumu wa malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s).

Majli hizo zimefanyika kwa muda wa siku tano mfululizo chini ya uhadhiri wa Shekhe Abdullahi Dujaili, amekua akiongea historia ya Imamu Hussein (a.s) na mambo muhimu yaliyotokea wakati wa uhai wake mtukufu.

Majlisi zilikua zinapambwa na tenzi za kuomboleza kifo cha bwana wa vijana wa peponi na yaliyo watokea watu wa nyumbani kwake (a.s) na wafuasi wake.

Atabatu Abbasiyya tukufu kwenye kila tukio linalo husu Ahlulbait (a.s), huandaa ratiba maalum ya kuomboleza kumbukumbu ya tukio hilo.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: