Zaidi ya mazuwaru (1700) wameshiriki kuandika msahafu mtukufu

Zaidi ya mazuwaru (1700) wameshiriki kuandika msahafu mtukufu kupitia vituo vya kutambulisha msahafu uliochapishwa na Atabatu Abbasiyya tukufu kwa simamiwa na Majmaa ya Qur’ani katika njia ya Yaa Hussein.

Mkuu wa kituo cha uchapishaji wa Qur’ani tukufu Shekhe Dhiyaau-Dini Zubaidi amesema “Kituo chetu kimehitimisha shughuli zake baada ya kukamilisha kuandika msahafu mtukufu katika maukibu ya Ummul-Banina (a.s) iliyopo barabara ya Najafu – Karbala.

Akaongeza kuwa “Wameshiriki mazuwaru wenye umri na jinsia tofauti wapatao (1751) kwenye uandishi wa msahafu mtukufu, mazuwaru wote waliojitokeza wamekutanishwa na mapenzi yao kwa kizazi kitakatifu na kitabu cha Mwenyezi Mungu mtukufu.

Kituo kilianzishwa kwa ajili ya kutambulisha msahafu ulioandikwa na Atabatu Abbasiyya tukufu hapa Iraq miaka nane iliyopita, nayo ni katika mafanikio makubwa ya kituo cha uchapishaji wa Qur’ani.

Akaendelea kusema “Milango ya kituo ilikua wazi (saa 24) kwa kila anaetaka kushiriki miongoni mwa mazuwaru wa Imamu Hussein (a.s)”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: