Atabatu Abbasiyya tukufu imesema: Idadi ya mazuwaru wa Arubaini ya Imamu Hussein (a.s) imefika zaidi ya milioni 21

Uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu leo Jumamosi mwezi (20 Safar 1444h) sawa na tarehe (17 Septemba 2022m), baada ya swala ya Adhuhuri, umetoa tamko rasmi la idadi ya mazuwaru waliosajiliwa kwenye mitambo maalum ya kuhesabu watu, imefika zaidi milioni ishirini na maoja laki moja tisini na nane elfu na mia sita arubaini (21,198,640).

Ifuatayo ni nakala ya tamko:

Tunatoa pole kwa Imamu wa zama Hujjat bun Hassan rehema za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake na juu ya wazazi wake na Maraajii watukufu, na ulimwengu wote wa kiislamu, hususan Iraq taifa la Mitume, Mawasii na Mawalii, katika kumbukumbu ya Imamu Hussein (a.s), tunamuomba Mwenyezi Mungu alinde miji ya kiislamu na kila baya, awarudishe mazuwaru wa Abu Abdillahi Hussein kwenye miji yao na mataifa yao wakiwa salama na wenye kukubaliwa ibada zao.

Kama kawaida yetu kwa zaidi ya karne 13, Mji wa Karbala umekua ukipokea mazuwaru wa bwana wa mashahidi Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) wakija kufanya ziara tukufu ya Arubaini, mwaka huu 1444h, ni utukufu kwetu kupokea na kuhudumia mazuwaru hao, tumetoa huduma za aina tofauti, zikiwemo huduma za kimatibabu (afya) na chakula, bila kusahau huduma ya kuwahesabu mazuwaru kwa kutumia mitambo maalum chini ya idara ya mawasiliano katika Atabatu Abbasiyya tukufu, huduma hii inatolewa kwa mwaka wa saba mfululizo.

Idadi ya mazuwaru waliowasiri katika mji mtukufu wa Karbala kuanzia mwezi mosi Safar hadi saa sita kamili (6:00) leo Adhuhuri imefika milioni ishirini na moja laki moja tisini na nane eflu mia sita arubaini (21,198,640) kwa mujibu wa mitambo ya kuhesabu watu iliyofungwa kwenye barabara ya (Najafu – Karbala, Baabil – Karbala, Husseiniyya – Karbala, Masaarin – Karbala).

Tunaandika idadi ya mazuwaru waliokuja miaka ya nyuma, tunamuomba Mwenyezi Mungu awakubalie wote ibada zao, na atuwafikishe katika anayopenda na kuridhia, hakika yeye ni mwingi wa kusikia mwingi wa kujibu.

Mwaka 1444 hijiriyya, (21,198,640) milioni ishirini na moja laki moja tisini na nane elfu mia sita na arubaini.

Mwaka 1443 hijiriyya, (16,327,542) milioni kumi na sita laki tatu ishirini na saba elfu mia tano arubaini na mbili.

Mwaka 1442 hijiriyya, (14,553,308) miloni kumi na nne laki tano hamsini na tatu elfu mia tatu na nane.

Mwaka 1441 hijiriyya, (15,229,955) milioni kumi na tano laki mbili ishirini na tisa elfu mia tisa hamsini na tano.

Mwaka 1440 hijiriyya, (15,322,949) milioni kumi na tano laki tatu ishirini na mbili elfu mia tisa arubaini na tisa.

Mwaka 1439 hijiriyya, (13,874,818) milioni kumi na tatu laki nane sabini na nne elfu mia nane kumi na nane.

Mwaka 1438 hijiriyya, (11,210,367) milioni kumi na moja laki mbili na elfu kumi mia tatu sitini na saba.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: