Kitengo cha utumishi kimesema kuwa hakikusimama kufanya usafi na kutoa huduma zingine wakazi wa ziara ya Arubaini pamoja na wingi wa mazuwaru.
Rais wa kitengo Sayyid Muhammad Aaraji, amesema kuwa kazi ya usafi haikusimama toka siku ya kwanza hadi leo pamoja na wingi wa mazuwaru ambao hutatiza upitaji wa mitambo ya kufanyia usafi na watumishi.
Akaongeza kuwa, tunafanya kazi kwa utaratibu maalum, tuna idadi kubwa ya watumishi walio ongezewa nguvu na watumishi wa kujitolea katika siku za ziara.
Baada ya kumaliza ziara na kubaki idadi ndogo ya mazuwaru, rais wa kitengo cha utumishi amesema kuwa utafanywa usafi mkubwa kwenye eneo lote linalo zunguka haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s) kwani mitambo ya usafi inatembea kwa urahisi.