Kitengo cha mgahawa kimesema: Bado tunaendelea kutoa huduma pamoja na kuisha kwa ziara ya Arubaini

Kitengo cha mgahawa katika Atabatu Abbasiyya tukufu kimesema kuwa, Pamoja na kuisha kipindi cha ziara ya Arubaini, bado kinaendelea kutoa huduma kwa mazuwaru hadi atakapo ondoka zaairu wa mwisho.

Rais wa kitengo hicho Mhandisi Aadil Jafari amesema “Kitengo cha mgahawa kimeongeza huduma zake baada ya kuisha kipindi cha ziara ya Arubaini kwa sababu ya kuondoka Mawakibu Husseiniyya nyingi zilizokua zikitoa huduma ya chakula katika mji wa Karbala”.

Akaongeza kuwa “Tunatarajia kupokea mazuwaru kutoka nchi tofauti duniani katika siku chache zijazo, hivyo kitengo cha mgahawa kitaendelea kutoa huduma ya chakula kwa wingi hadi mwisho wa mwezi huu wa Safar”.

Kuhusu vituo vya kugawia chakula amesema “Kutakua na vituo saba ndani ya eneo la mji wa Karbala, kwenye barabara ya Abulfadhil Abbasi (a.s), eneo la mlango wa Bagdad, karibu na Maqaam ya Imamu wa Zama (a.f) na pembeni ya mgahawa”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: