Atabatau Abbasiyya yafanya majlisi ya kuomboleza kumbukumbu ya Arubaini ya Imamu Hussein (a.s)

Uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu jioni ya Jumapili, umefanya majlisi ya kuomboleza Arubaini ya Imamu Hussein (a.s) ndani ya ukumbi wa utawala, iliyohudhuriwa na wahudumu wa malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s).

Majlisi ilifunguliwa kwa Qur’ani tukufu na itadumu kwa muda wa siku tatu, baada ya Qur’ani ukafuata muhadhara uliotolewa na Shekhe Abdullahi Kaabi, ameongea kuhusu uhai wa Imamu Hussein (a.s) na mambo muhimu yaliyotokea katika historia yake.

Majlisi ikahitimishwa kwa utenzi uliosomwa na Ali Basha Karbalai, uliotaja huzuni za waumini katika kumbukumbu ya Arubaini ya bwana wa vijana wa peponi na yaliyo watokea watu wa familia yake na wafuasi wake (a.s).

Atabatu Abbasiyya tukufu kwenye kila tukio linalohusu kumbukumbu ya kifo fa Ahlulbait (a.s) huandaa ratiba ya kuomboleza tukio hilo.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: