Zaidi ya watu elfu 10 waliopotea wakati wa ziara ya Arubaini wamerudishwa kwa jamaa zao na Atabatu Abbasiyya tukufu

Vituo vya kuongoza waliopotea vinavyo simamiwa na Atabatu Abbasiyya tukufu vimefanikiwa kuwakutanisha na jamaa zao watu waliokuwa wamepotea (10726) wakati wa ziara ya Arubaini.

Kiongozi mtendaji wa mradi huo bwana Muntadhiru Swadiq amesema “Atabatu Abbasiyya tukufu kupitia vituo vya kuelekeza waliopotea imefanikiwa kuwakujanisha na jamaa zao watu walikua wamepotea (10726) elfu kumi miasaba ishirini na sita, kuanzia mwezi 11 hadi 21 Safar”, akafafanua kuwa “Vituo hivyo vimetumia njia zote zilizoandaliwa katika kutekeleza jukumu lao”.

Idara ya mahusiano chini ya kitengo cha mahusiano katika Atabatu Abbasiyya, ilichukua jukumu la kusimamia vituo vya kuongoza waliopotea, jumla wa wanafunzi (450) wameshiriki kutoa huduma kwa kujitolea kwenye vituo hivyo.

Vituo vilikua maeneo matatu, na jumla kulikua na vituo (40), upande wa Najafu, upande wa Hilla, upande wa Bagdad na vituo vingine viliwekwa ndani ya mji wa Karbala, aidha kulikua na vikundi (15) vya waelekezaji wanaozunguka.

Akaongeza kuwa “Wairaq waliopotea walirudishwa kwa jamaa zao moja kwa moja kwa kupitia simu au anuani zao, na wageni kutoka nje ya nchi walikabidhiwa kwenye balozi zao au balozi ndogo baada ya kushidhwa kupata jamaa zao”.

Akafafanua kuwa: Njia za kupata taarifa, tulitumia simu, matangazo, mitandao, App ya Haqibatu Mu-uminu, au huduma ya kuelekeza waliopotea, njia zote zilikua zimeunganishwa na kituo kikuu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: