Maktaba ya Ummul-Banina (a.s) imesema kuwa, imeweka mkakati wa baada ya kumaliza kutoa huduma za ziara ya Arubaini, kwa lengo la kupanua wigo wa utendaji.
Kiongozi wa maktaba chini ya kitengo cha Habari na utamaduni bibi Ibtisam Atwaa amesema “Hema huwekwa kila mwaka katika ardhi ya chuo kikuu cha Al-Ameed upande wa (Najafu/ Karbala)” akaongeza kuwa “Hakika Maukibu ya Ummul-Banina (a.s) mwaka huu imetoa huduma nyingi zaidi kwa muda wa siku saba mfululizo”.
Akabainisha kuwa “Zimeelezwa shughuli zinazofanywa na maktaba ya Ummul-Banina kwa mazuwaru wa Imamu Hussein (a.s) wanaokuja kwenye kumbukizi ya Arubaini kutoka kila sehemu ya dunia”.
Kwa mujibu wa kiongozi wa maktaba, wanufaika wa huduma zetu ni maelfu ya mazuwaru, juhudi zinaendelea za kupanua wigo wa huduma na kuwafikia mazuwaru wengi zaidi miaka ijayo.