Kitengo kinachosimamia uwanja wa katikati ya haram mbili tukufu kinafanya usafi mkubwa katika eneo la mji wa zamani ndani ya mkoa wa Karbala

Watumishi wa kitengo kinachosimamia uwanja wa katikati ya haram mbili tukufu katika Atabatu Abbasiyya, wanafanya kazi kubwa ya kusafisha mji wa zamani, baada ya kumajiza msimu wa ziara ya Arubaini katika mji wa Karbala.

Makamo rais wa kitengo hicho Sayyid Hamdu Shaakir Hashim amesema “Toka ilipoanza ziara tukufu hadi sasa, watumishi wetu wanafanya kazi kubwa ya kusafisha barabara na maeneo yote yanayozunguka Atabatu Abbasiyya tukufu, hususa eneo la mji wa zamani”.

Makamo rais wa kitengo hicho akaendelea kusema kuwa, watumishi wa kitengo kinacho simamia uwanja wa haram mbili tukufu wanafanya usafi mkubwa baada ya kumaliza ziara ya Arubaini, maeneo wanayo safisha ni (Mlango wa Bagdad, barabara ya Hauraa Zainabu, barabara ya Alqami, barabara ya Jannatul-Hussein, barabara ya maosheo ya zamani, eneo la katikati ya haram mbili tukufu, barabara ya Maimamu).

Akaendelea kusema “Hadi leo tumesha ondoa tani (90/ 100) za taka, kazi hii tunafanya kwa kushirikiana na wahudumu wa kujitolea pamoja na idara ya mji mtukufu wa Karbala”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: