Majmaa ya Qur’ani tukufu imesema: vituo 70 vya kufundisha usomaji vimetoa huduma wakati wa ziara ya Arubaini

Majmaa ya Qur’ani chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu imesema kuwa, kulikua na vituo sabini vya kufundisha usomaji sahihi wa Qur’ani kwenye barabara zilizokua zikitumiwa na mazuwaru wengi waliokuja kufanya ziara ya Arubaini.

Mkuu wa Maahadi ya Qur’ani tukufu chini ya Majmaa Shekhe Jawadi Nasrawi amesema “Zaidi ya vituo (70) vya kufundisha usomaji sahihi wa Qur’ani vilifunguliwa kwenye barabara zinazoelekea Karbala, na vimetoa huduma tofauti zinazohusu Qur;ani”.

Akaongeza kuwa: “Kupitia vituo hivyo tumejitahidi kufikia malengo tofauti, miongoni mwa malengo hayo ni kujenga utamaduni wa kusoma Qur’ani katika jamii na matembezi ya kwenda kwa bwana wa mashahidi (a.s)”.

Vituo vimetoa huduma siku zote za ziara, akasema kuwa “Jambo kubwa katika huduma tulizotoa lilikua ufundishaji wa Qur’ani kwa mazuwaru, vikao vya usomaji wa Qur’ani, mashindano ya kielimu, ushiriki wa mahafidhu kutoka Maahadi, aidha tumegawa machapisho 300,000 kwa mazuwaru”.

Akasema: “Vituo vya ufundishaji wa usomaji sahihi wa Qur’ani tukufu vimejitahidi kufikia idadi kubwa ya mazuwaru, vilikua na jumla ya wakufunzi (470) na wamekua wakifundisha kila siku kwenye vituo hivyo, vilivyo wekwa katika mikoa ya (Basra, Dhiqaar, Misaan, Muthanna, Diwaniyya, Waasit, Bagdad, Baabil na Karbala)”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: