Hema la Naafidhul-Baswirah limesajili zaidi ya wanufaika elfu 16 katika ziara ya Arubaini

Hema la Naafidhul-Baswirah lililoandaliwa na kitengo cha Habari na utamaduni limesema kuwa zaidi ya watu elfu (16) wamenufaika kwenye hema hilo wakati wa ziara ya Arubaini.

Wasimamizi wa hema hilo ni kituo cha tafiti na marejeo ya kielimu kwa mujibu wa mkuu wa kituo Sayyid Hassan Aljawadi, amesisitiza kuwa “Hema lilifungwa kwenye barabara ya Najafu - Karbala, Bagdad - Karbala, pamoja na kwenye haram tukufu ya Abulfadhil (a.s) na katikati ya mji wa Karbala, wanufaika walifika mazuwaru (16175)”.

Akasema kuwa “Hema la Naafidhul-Baswirah linalenga kutoa elimu na utamaduni, sambamba na kufuata mwenendo wa mwezi wa familia Abbasi bun Ali (a.s) ndio maana ya kutumia jina lake la (Naafidhul-Baswira)”.

Hema lilikua na vituo vine, ambavyo ni: “kituo cha (mimi na Ashura), kituo cha (mimi na jamii), kituo cha (mimi na simu) nacho ni kituo cha mawasiliano pamoja na mazuwaru, sambamba na kueleza matumizi ya simu ganja, na kujiepusha na kutumia muda mwingi kwenye intanet, na kituo cha (mimi na kitabu), nacho ni kituo kilichokua kinahimiza mazuwaru wanaokwenda Karbala kujenga utamaduni wa kusoma vitabu”.

Akasema kuwa: “Katika siku za ziara ya Arubaini tumegawa zaidi ya machapisho tofauti elfu saba, na tumetoa mihadhara (7) sambamba na kufanya vikao vya mazungumzo na mazuwaru”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: