Uongozi wa jengo la Alqami umesema: Tumetoa zaidi ya sahani laki mbili za chakula wakati wa ziara ya Arubaini

Uongozi wa jengo la Alqami umetangaza kuwa, wamegawa zaidi ya sahadi za chakula laki mbili (200,000) kwa watu waliokuja kufanya ziara ya Arubaini katika mji mtukufu wa Karbala.

Rais wa jengo hilo Sayyid Ali Niimah Alkhafaji amesema “Tulianza kutoa huduma kwa mazuwaru mwezi saba Safar, tulikua tukihudumia zaidi ya watu elfu nne kila siku”.

Akaongeza kuwa “Tulizingatia ugawaji wa chakula katika milo mitatu mikuu, ambayo ni chakula cha asubuhi, mchana na jioni, sambamba na kugawa maji ya kunywa, juisi na vitanwa, ndani ya siku (11) tumegawa zaidi ya sahani laki mbili za chakula”.

Akasema kuwa “Idadi ya mazuwaru ilikua inaongezeka kila siku hadi tulifikia kulaza watu elfu tano kwa siku”.

Akafafanua kuwa “Tumefanikiwa kuhudumia mazuwaru wote kutokana na msaada wa watoa huduma wa kujitolea” akasisitiza kuwa “Kuna umuhimu wa kweka mkakati wa kuhakikisha kumbi zote zinakua na viyoyozi kwani ziara ya mwakakesho inatarajiwa kuwa wakati wa joto”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: