Kamati ya majaji wa shindano la (zawadi ya vizito viwili) imesema: zimekaguliwa nyaraka za washiriki na matokeo ya awali yatatangazwa hivi karibuni

Kamati ya majaji wa shindano la (zawadi ya vizito viwili) linalo husu maandishi ya Msahafu mtukufu imesema kuwa, imekagua nyaraka za washiriki na matokeo ya awali yatatangazwa ndani ya wiki mbili zijazo.

Mkuu wa kituo cha kuchapisha Qur’ani tukufu Shekhe Dhiyaau-Dini Zubaidi amesema: “Kamati ya majaji ilianza kazi ya kupitia nyaraka za washiriki, toka ulipoisha muda wa kukabidhi nyaraka hizo za shindano la kwanza la zawadi ya vizito viwili, linalo husu maandishi ya msahafu, nyaraka hizo zimewasilishwa kwenye kituo cha uchapishaji wa Qur’ani chini ya Majmaa ya Qur’ani tukufu katika Atabatu Abbasiyya”.

Akaongeza kuwa “Kazi inaendelea ya kuchagua nyaraka kumi bora, waandishi wa nyaraka hizo wataitwa na kila mmoja atapewa kazi ya kuandika juzuu tatu”.

Akasema kuwa “asilimia kubwa ya washiriki wanatoka kwenye mikoa ya Bagdad, Dhiqaar, Baabil, Najafu, Karkuuk, Waasit, Ambaar, Arbiil, Karbala, Misaan, Suleimaniyya, Basra, Diwaniyya na Nainawa”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: