Baada ya kumaliza ziara.. kitengo kinachosimamia uwanja wa katikati ya haram mbili kinaondoa vizuwizi vilivyo wekwa kwa muda kwenye barabara

Baada ya kumaliza ziara ya arubaini watumishi wa kitengo kinachosimamia uwanja wa katikati ya haram mbili tukufu wameanza kuondoa vizuwizi vilivyo wekwa kwa muda kwenye barabara zinazo elekea katika eneo hilo ili kuongoza matembezi ya mazuwaru.

Rais wa kitengo hicho Sayyid Naafii Mussawi amesema “Baada ya kumaliza ziara na kupungua idadi ya mazuwaru, watumishi wa kitengo chetu wameanza kuondoa vizuwizi vilivyowekwa kwenye barabara kwa ajili ya kuongoza matembezi ya mazuwaru na kuondoa msongamano wakati wa ziara ya Arubaini”.

Akaongeza kuwa “Tulitumia vizuwizi vya plastiki kugawa barabara zinazo zunguka malalo tukufu, tukafanya upande mmoja wa watu wanaoingia na mwingine wanaotoka, kutokana na wingi wa mazuwaru wa Arubaini waliokuja kutoka mikoa yote ya Iraq na kila sehemu ya dunia”.

Kwa mujibu wa maelezo ya rais wa kitengo “baada ya kila ziara kubwa watumishi wetu hufanya usafi mkubwa, kwa ajili ya kurudisha mazingira katika hali ya kawaida sambamba na huduma zingine”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: