Kituo cha Dirasaati Afriqiyya kimeshiriki kwenye kongamano la tatu la ujumbe wa Hussein (a.s)

Ujumbe kutoka Markazi Dirasaati Afriqiyya umeshiriki kwenye kongamano la ujumbe wa Hussein (a.s) linalofanywa kwa mwaka wa tatu, ambalo linalenga mazuwaru wa Iraq kutoka nchi za kigeni, lililoandaliwa na Atabatu Husseiniyya katika mji wa Karbala.

Kiongozi wa idara ya Tablighi katika Markazi hiyo chini ya kitengo cha Habari na utamaduni Sayyid Muslim Aljabiri amesema: “Ushiriki wetu kwenye kongamano hili umetupa uzowefu wa mambo mengi yanayo husu namna ya kuratibu Tablighi na shughuli za kibinaadamu katika bara la Afrika kwa maslahi ya Ahlulbait (a.s) wanao ishi huko”.

Kongamano hilo limehudhuriwa na wawakilishi wa wafuasi wa Ahlulbait (a.s) kutoka nchi tofauti duniani zikiwemo nchi za Afrika.

Akaongeza kuwa: “Kongamano lilitoa nafasi ya kusikiliza wawakilishi wa Ahlulbait (a.s) kutoka nchi za Afrika na nchi za Asia, ambao wameongea mambo muhimu”, akasema “Nimefanya mazungumzo na wawakilishi kutoka Arfika pembeni ya kongamano hilo na kuangalia namna ya kufikisha ujumbe wa Imamu Hussein (a.s) katika mataifa yao”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: