Atabatu Abbasiyya imesema: Lita milioni 63 za maji zimetumika wakati wa ziara ya Arubaini

Kitengo cha miradi ya kihandisi katika Atabatu Abbasiyya tukufu kimesema kuwa lita milioni (63) za maji zimetumika wakati wa ziara ya Arubaini katika mji wa Karbala.

Kiongozi wa idara ya maji Mhandisi Basaam Hashimiy amesema: “Kituo cha usambazaji wa maji katika Atabatu Abbasiyya kimetekeleza wajibu wake kwenye ziara ya Arubaini, kimesambaza lita milioni (63) za maji, akabainisha kuwa maji yametumika sehemu tofauti, kutawadha, kunywa, vyooni..”.

Akaongeza kuwa “Wtumishi wa kituo walifanya kazi ya kusambaza maji kwenye haram tukufu, uwanja wa katikati ya haram mbili, na maeneo jirani saa (24) kila siku”.

Akafafanua kuwa: “Kituo cha (RO) kilisambaza maji lita milioni moja na yaki mbili na elfu hamsini hadi milioni moja na laki tano kila siku”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: