Kitengo cha maadhimisho na mawakibu Husseiniyya kimesema kuwa kilifanikiwa kusimamia matembezi ya mawakibu Husseiniyya zilizoshiriki kwenye ziara ya Arubaini.
Rais wa kitengo hicho chini ya Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya Sayyid Aqiil Alyaasiriy amesema “Mawakibu Husseiniyya zilikua zinaingia kupitia mlango mkuu wa upande wa barabara ya Kibla ya Imamu Hussein (a.s), kisha wanapita kwenye uwanja wa katikati ya haram mbili na kuishia katika malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s), akafafanua kuwa kila maukibu iliingia kwa kufuata muda waliopangiwa, tulianza na mawakibu za Zanjiil na tukamalizia kwa mawakibu za matam, zowezi hilo lilidumu kwa muda wa siku tano”.
Akaongeza kuwa “Ziara ya mwaka huu imeshuhudia ongezeko la mawakibu, inatokana na kutokuwepo kwa ushiriki wao miaka miwili iliyopita kwa sababu ya janga la Korona, tambua kuwa watumishi wa kitengo cha maadhimisho walisimamia matembezi ya mawakibu siku zote”.
Akasisitiza kuwa “Mkakati wa kitengo umefanikiwa kwa kushitikiana na vitengo vingine, matembezi yamefanyika kwa amani na utulivu bila kusababisha msongamano wowote”.
Kuhusu ushiriki wa mawakibu kutoka nchi za kiarabu na kiajemi, “mwaka huu kumekua na ongezeko la idadi ya mawakibu zao, pia kulikua na maukibu za pamoja, kwa mfano maukibu ya Baharain, maukibu ya Saudia na maukibu zingine moja moja, tunatarajia mwakani ziungane na kuwa na maukibu za pamoja, kwa mujibu wa maoni ya rais wa kitengo”.