Majmaa ya Qur’ani tukufu katika Atabatu Abbasiyya imekamilisha maandalizi ya kufungua viuo vitano vya Qur’ani kwenye eneo la katikati ya mji wa Najafu na pembezoni mwake, wakati wa kumbukumbu ya kifo cha Mtume Muhammad (s.a.w.w) mwezi (28) Safar.
Vituo hivyo vitasimamiwa na Maahadi ya Qur’ani tukufu chini ya Majmaa ya Qur’ani kwa mujibu wa mkuu wake Sayyid Muhandi Almayali “Idara ya usomaji wa Qur’ani imekamilisha maandalizi ya kufungua vituo vitano vya Qur’ani katika njia zinazotumiwa na mazuwaru waenda kwa miguu kwenye malalo ya kiongozi wa waumini (a.s) kuomboleza kifo cha Mtume Mtukufu (s.a.w.w)”.
Akasema: “Jukumu la vituo hivyo ni kusahihisha usomaji wa Qur’ani kwenye sura fupi na kufafanua baadhi ya hukumu za swala sambamba na kutoa huduma zingine kwa mazuwaru”.
Kuhusu sehemu zitakazo wekwa vituo hivyo kiongozi wa idara ya usomaji Sayyid Ahmadi Zaamiliy amesema: “Wilaya ya Mashkhabu, Mtaa wa Huriyya, Mtaa wa Radhawiyya na Mtaa wa Abbasiyya, kutakua na wasimamizi 25 ambao ni walimu, wasomaji na mahafidhi, kituo kukuu kitakua kwenye uwanja wa Thauratul-Ishrin, kikiwa na zaidi ya wasimamizi 20 ambao ni wasomaji na mahafidhi kutoka Maahadi”.